Radio Furaha 96.7 FM

KUTANGAZA INJILI KWA WATU WOTE


ALPHA AWA RAIS MPYA GUINEA

image

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Guinea imemtangaza Alpha Conde kuwa Rais wa Guinea, baada ya kushinda uchaguzi mkuu ambao umefanyika Jumapili iliyopita ambapo ameshinda kwa asilimia 58 ya kura zote.

Tume ya uchaguzi ya Guinea, imetangaza matokeo hayo ya uchaguzi ambapo rais Conde ataanza rasmi muhula wake wa pili bila ya kuwa na marudio ya uchaguzi huo mkuu.

Aidha, matokeo hayo yamepingwa na viongozi wa upinzani.
Kinara mkuu wa upinzani Cellou Dalein Diallo, alijiondoa katika uchaguzi huo Jumatano iliyopita akidai kuwa ulikumbwa na udanganyifu.

Kiongozi huyo wa upinzani sasa ameitisha maandamano ya amani kupinga matokeo hayo.

Waangalizi wa  kimataifa waliokuweko huko wamesema kumejitokeza mapungufu kidogo siku ya upigaji kura, lakini hayakuwa mkubwa kiasi cha kutatiza matokeo ya uchaguzi huo.


MISRI WAANZA KUPIGA KURA ZA WABUNGE

image

Shughuli za upigaji kura kuwachagua wabunge zinaanza rasmi leo Jumapili Misri na katika balozo zote za nchi hiyo .
Huu ndio mkondo wa kwanza wa uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu ya kuwachagua wawakilishi wa ubunge.
Wengi wa wagombeaji ni waungwaji mkono wa rais wa zamani na kamanda mkuu wa jeshi, Abdul Fattah al-Sisi.
Kundi kubwa zaidi la kiislamu la The Muslim Brotherhood — halikubaliwi kugombea katika uchaguzi huo.
Kilishinda uchaguzi uliopita wa ubunge miaka mitatu iliyopita.
Hata hivyo vuguvugu hilo lilipigwa marufuku baada ya jeshi kutwaa utawala mnamo mwaka wa 2013.
Kuna mikondo miwili ya upigaji kura huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutangazwa mapema mwezi Disemba.
Uchaguzi wa ubunge umesubiriwa kwa muda mrefu nchini Misri.


BLATTER ASIMAMISHWA FIFA

image

RAIS wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou kutoka Cameroon amepewa jukumu la kuongoza shirikisho la soka duniani Fifa kwa muda.
Hayatou atachukua usukani kufuatia kusimamishwa kazi kwa Rais wa Fifa Sepp Blatter kwa muda wa siku 90 na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo, shirikisho hilo linalosimamia soka duniani limesema kupitia taarifa.
Hayatou, aliyeongoza CAF tangu 1988, atachukua usukani kwa mujibu wa sheria za Fifa, akiwa ndiye makamu wa rais katika kamati tendaji ya Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi.
Baadaye, Hayatou ametoa taarifa na kusema amepokea majukumu hayo mapya lakini ataongoza tu kwa muda.
“Rais mpya atachaguliwa kwenye Mkutano Mkuu Februari 26, 2016. Na mimi mwenyewe sitawania,” amesema kupitia taarifa.
“Hadi mkutano huo ufanyike, naahidi kwamba nitajitolea kwa nguvu zangu zote kutumikia shirikisho hili, mashirikisho wanachama, waajiri wetu, washirika na mashabiki wa soka popote walipo.”
Aidha, ameahidi kuendelea kushirikiana na watawala na kuendeleza uchunguzi kwenye shirikisho hilo lililoyumbishwa na madai ya ulaji rushwa.


WAFUASI WA CHADEMA IRINGA WAWEKWA NDANI

https://fbcdn-sphotos-b-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xap1/v/t1.0-9/11051776_907704475943533_1837842231222341305_n.jpg?oh=18ba28e42c67ff4ecbd94afa96db86c7&oe=56637EE1&__gda__=1446673725_69d7d3d0a1f231c5ce32355103de477a

Wafuasi wa Chama cha Demokrasia wawekwa chini ya ulinzi baada ya kusadikika kutaka kuleta Vurugu maeneo ya Sambala kwenye ofisi zao za mkoa hapo jana jioni. Mpaka asubuhi ya leo walikuwa kizuizini chini ya ulinzi na biashara za Soko kuu lilopo karibu na Kituo cha polisi kikisitsha huduma kutokana na vurugu zilizokuwa zikiendelea


Lowasa ajaza watu Tanga

 

Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakimlaki kwa shangwe Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Kisiwani, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo jana Septemba 28, 2015.

 

 


Wakenya na Watanzania walifariki Mecca

Mahujaji watatu kutoka Kenya ni miongoni mwa watu 717 waliofariki baada ya mkanyagano kutokea karibu na mji wa Mecca, Saudi Arabia, afisa wa serikali ya Kenya amesema.

Majeruhi Mecca

Bw Washington Oloo, afisa wa wizara ya mashauri ya kigeni anayehusika na masuala ya Wakenya wanaoishi ng’ambo amesema Mkenya mwingine mmoja aliumia na amelazwa hospitalini. Mahujaji wanane bado hawajulikani waliko.

Nchini Tanzania kiongozi mmoja wa Kiislamu nchini humo amesema wamethibitisha kuwa raia wanne wa Tanzania walifariki katika mkasa huo uliotokea Alhamisi.

“Nimepokea taarifa za majeruhi miongoni mwa mahujaji wetu wa Tanzania na baadhi ya majeruhi nimeonana nao mara baada yao kuruhusiwa kuondoka hospitalini,” amesema mufti wa Tanzania Sheikh Abu Bakari Zuberi aliye Mecca, kupitia taarifa aliyoituma kwa vyombo vya habari.

“Katika kipindi hiki cha taharuki kubwa, tunafanya mawasiliano na wizara husika hapa Saudi Arabia.”

Alisema maafisa wa Saudia bado wanaendelea kutambua uraia wa waliofariki.

Mkanyagano ulitokea eneo la Mina mahujaji walipokuwa wakielekea kwenye nguzo za Jamaraat.

Mahujaji husafiri kila mwaka hadi Mina wakati wa kuhiji kurusha mawe saba kwenye nguzo saba zijulikanazo kama Jamarat, ambazo huwakilisha shetani.

Nguzo hizo zimo katika eneo ambalo inaaminika Nabii Ibrahim alijaribiwa na shetani.

Idara ya ulinzi wa raia Saudi Arabia imesema mkanyagano huo ulitokea pale kulipotokea “ongezeko la ghafla” la watu waliokuwa wakielekea kwenye kwenye nguzo hizo.

Waziri wa afya wa Saudi Arabia Khaled al-Falih amesema mkanyagano huo ulitokea kwa sababu mahujaji walikosa kufuata maagizo.

“Wengi wa mahujaji huenda bila kufuata ratiba iliyowekwa,” amesema.

CHANZO bbc